Luke 17:26-29

26 a“Kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku za Mwana wa Adamu. 27 bWatu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Nuhu alipoingia katika safina. Ndipo gharika ikaja na kuwaangamiza wote.

28 c“Ndivyo ilivyokuwa katika siku za Lutu: Watu walikuwa wakila na kunywa, wakinunua na kuuza, wakilima na kujenga. 29 dLakini siku ile Lutu alipoondoka Sodoma, ikanyesha mvua ya moto na kiberiti kutoka mbinguni ukawaangamiza wote.

Copyright information for SwhKC